Wednesday, February 15, 2012

IFAHAMU HISTORIA YAKO KABLA YA KUWA MTUMWA KWENU

Mambo vip wadau wa blog yetu...?? Natumaini weekend yenu ilikwenda vizuri na tuko na afya njema pamoja na wenzetu tuwapendao. Kama kuna mtu anaumwa au kuuguliwa na ampendaye basi tunawaombea ahueni ili tuendeleze gurudumu la maendeleo la maisha yetu binafsi, wanaotuzunguuka na taifa letu kwa ujumla.
Siku ya jumamosi nilipata wasaa wa kwenda kutembelea mji wa bagamoyo na kujua historia mbalimbali za mji ule... Kuna vitu vingi sana nilijifunza kupitia safari yangu hii na pia kuupata huo usemi uliokuwa hapo juu wa IFAHAMU HISTORIA YAKO KABLA YA KUWA MTUMWA KWENU.
Kitu cha kwanza baada ya kufika bagamoyo, ilikuwa mida ya swala kwahiyo nikakimbilia msikitini uliopo pichani hapo juu nikapata jama'a pale kisha nikaelekea zangu D'Z restaurant kupata chochote kitu kabla ya kuanza kuchimbua historia ya mji huo.
Hii ndio lunch nilioipata hapo D'z restaurant kisha nikaelekea moja kwa moja mpaka CROCODILE BRANCH. Hili ni eneo ambalo wanafuga mamba wa ukubwa na umri mbalimbali.. kuanzia umri wa siku moja mpaka mamba mkubwa kabisa ambae nimemshuhudia mwenye umri wa miaka 52 ambae alikamatwa kwenye mto pangani mwaka 1998 akiwa tayari ameishi miaka 38 duniani.
Nikiwa njiani kuelekea huko CROCODILE BRANCH nilipitia kwanza CARAVAN SERAI MUSEUM ambayo ipo katikati ya mji kabisa ambapo ndipo alipokuwa akikaa wakala/agent wa waarabu wa watumwa waliokuwa wakitoka maeneo tofauti nchini kabla ya kupakiwa kwenye mitumbwi kwenda Zanzibar.


Baada ya museum ndio nikaenda zangu kuona hawa wanyama wa ajabu ambao wanaishi mpaka miaka 150 duniani. Siri moja niliyopewa hapa ni kwamba kumbe mamba akishikwa kichwani vizuri na mkiani ujanja tena unakuwa mfukoni.. Hahahahaaa, nilijifunza mengi tuu na hawa jamaa hivi karibuni wataongeza wanyama wengine kama simba, twiga, nyoka na kadhalika. Itapunguza visingizio vya watu kushindwa kwenda kufanya utalii wa ndani kwa visababu kama vya umbali na gharama.


Nilipata nafasi na mie kushika mamba.. Uoga wangu wote niliuweka mfukoni.

Huyu ndio jamaa aliyekuwa anatuzunguusha na kutupa maelezo kuhusu hawa mamba... Hawa majamaa, wakubwa wanakula mpaka kilo 450 za nyama kwa wiki. Heeeeeeeh... Nikasema bora na me niwe mamba ili niweze kugonga nyama za kutosha tuuuu.
Huyo jamaa aliyevaa jersey ya barcelona ndio alikuwa mwenyeji wangu, anaitwa Jumanne.. Alinipa story nyingi sana za mtaani kwao na maisha ya ujumla ya vijana wa pale pamoja na changamoto wanazozipata kama vijana. Kwa kweli alinifungua macho kwenye mambo mengi na tukakubaliana next time nikienda tuonane ili tuongelee kwa upana zaidi maisha ya kawaida..

Baada ya CROCODILE BRANCH nikaelekea zangu hapa, kwenye magofu ya KAOLE. Hapa nilipata hasaa historia ya bagamoyo kwamba makabila asilia hapa ni WAKWERE( kabila la Mr. President), WAZARAMO na WADOE lakini kutokana na muingiliano wa kindoa na kimazingira kuna makabila kama WAZIGUA( akina sie sasa hawa) pia wapo mji huuu pamoja na makabila mengine. Neno KAOLE limetokana na lugha asilia ya wakwere " Shite shikalole" likimaanisha twende tukaone.. Wakati huo walikuwa wakija eneo hili kuja kuwashangaa WASHIRAZI walipokuwa wakiadhini kwa kupaza sauti wakati wa swala. WASHIRAZI walishindwa kusema "shite shikalole" wakaishia kusema KAOLE pekee.

Huu ndio msikiti wa WASHIRAZI amabao ulijengwa karne ya 13 na ndio uliokuwa unakuja kushangawa na makabila wenyeji wa bagamoyo. Hizo ngazi unazoziona hapo mbele ndio sehemu ambayo mtu akitaka kuadhini anapanda juu na kutoa adhana.


Hili ni kaburi la DARWESH.. Hili si jina halisi la aliyezikwa hapa, bali ni cheo alichokuwa nacho. DARWESH maana yake ni kiongozi wa mstari wa mbele kwenye mapambano ya kueneza dini ambayo ilikuwa uislamu kwa WASHIRAZI.


Hiki ndio kisima al-maarufu sana cha SHARIFA na si SHARIFU kama wengi wetu tulivyokuwa tukisikia. Kisima hiki watu huja kunywa maji yake na wengine kuoga ili kuondoa mikosi na balaa maishani mwao. Kisima hiki hakijawahi kukauka tangu kujengwa kwake karne ya 13 na ajabu zaidi ni kwamba kinatoa maji baridi(yasiyokuwa na chumvi) japokuwa kimechimbwa kandokando ya bahari. Umaarufu zaidi pia ni kutokana na historia ya SHARIFA mwenyewe ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 13 na alikuwa ni mtabiri wa mambo mbalimbali. Siku aliyofariki, walifariki pia watoto wengine watatu ikiaminika kwamba walikuwa wakimsindikiza SHARIFA.





Hili ndio kaburi la SHARIFA( lilijengwa kama nyumba) pembeni likiwa limezungukwa na makaburi ya hao watoto wengine watatu waliomsindikiza.

Hili ni kaburi la Sheikh Ali bin Jumaa amabaye alizaliwa mwaka 1215 na kufariki 1270. Huo kama mlingoti mbele ya kaburi ulikuwa ukijengwa kama ishara ya cheo ulichonacho kwenye jamii. Jinsi huo mlingoti unavyokuwa mrefu ndio inaonesha jinsi gani cheo cha mtu.


Kaburi la wapendanao hilo... Watu huja pia hapa na kuomba dua wakiamini kupata baraka kwenye ndoa zao na mahusiano yao pia.


Huu ni msingi wa nyumba iliyojengwa na washirazi karne ya 13.. Ilichimbuliwa tena na muingereza aliyeitwa Dr. Neville Chirtick mwaka 1958.


Huu ni msikiti mwingine wa washirazi.. Ulijengwa karne ya 15


Nikaenda pia MSALABANI.. Hii ilikuwa ni alama iliyowekwa na wakatoliki wakat walipokuwa wamejenga kanisa lao la kwanza la kikatoliki afrika mashariki


Na hili ndio kanisa lenyewe


Huu ni mbuyu ulipandwa kama alama ya ufunguzi wam kanisa hili la wakatoliki.. Ulipandwa mwaka 1868 na pia ni maarufu kwa kuwa umekuwa ukiongezeka upana na hadi mara ya mwisho kupimwa ulikuwa na upana zaidi ya mita 12. Pia kuna mnyororo ambao ulitumika kufungia punda karne hiyo..


Wakati nikiwa kwenye safari yangu hii ya kuchimbua historia, pia nilipata bahati ya kukumbana na DINA MARIOS mtangazaji maarufu wa clouds fm akifanya shooting ya kipindi chake cha LEO TENA. Hatukuongea kwasababu nilimkuta yupo kati kati ya shooting lakini nilipenda kupata wasaa tukabadilishana mawili matatu maana nae kama kijana nadhani angeweza kutusaidia mchango wa mawazo namna ya kuimarisha blog yetu.

Kwa picha zaidi ya safari hii yangu ya BAGAMOYO.. Tafadhali tembelea ukurasa wangu wa facebook kisha angalia photos zangu kwenye albamu ya BAGAMOYO EXPLORATION utapata zilizobaki ambazo sikupata muda wa kuziweka hapa.

Shukrani sana kwa mshkaji wangu JUMANNE... Aliniwezesha sana kupata burudani ya bagamoyo.

STAY TUNED.... KUNA TRIP YA TANGA NA ZANZIBAR, PHOTOS ZITAKUJA HAPA AS SOON AS POSSIBLE BAADA YA SAFARI HIZO.!!!!!



Thursday, February 9, 2012

HAMNA WATU WABUNIFU KAMA SISI WAAFRICA,SIJUI KWANINI HATUENDELEI

MAAZIMIO YA KIKAO KATI YA WAZIRI MKUU NA MADAKTARI JANA


Kamati ya muda ya kushughulikia madai ya madaktari nchini inapenda kuwajulisha madaktari wote pamoja na kada nyingine zote za afya nchini juu ya kile ambacho kimejiri katika siku ya leo ya tarehe 09.02.2012 ikiwa ni matokeo ya kikao wanataaluma wa kada za afya na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda na baadaye kufuatiwa na kikao kati ya madaktari na kada nyingine za afya.

Thursday, February 2, 2012

MADAWA YA KULEVYA NI HATARI KWA AFYA YAKO PAMOJA NA MAISHA YAKO..KUWA MUANGALIFU

Nasir and Salum
Nasir Husein kushoto..kijana ambye alikua mtanashati na smart sana kipindi cha nyuma,ila kwa sasa tumempoteza na sio kama alivyokua hapo nyuma.Mimi kama mshikaji wake na mate wake kila napo muona pale Ilala Boma Kituoni huwa inaniuma sana sana ndugu zangu.Napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha kuwa Madawa ya kulevya sio issue,jaribu kutafuta kitu cha kufanya ambacho kitakusaidia maishani mwako mbeleni na si kutafuta/kufanya kitu ambacho kitakuharibia maisha yako ya mbeleni

WADAU WA GILMAN RUTIHINDA ALUMNI..KATIKA KIKAO CHA KUUNDA KATIBA

                                          Dada Rehema,Joseeeeee,Joseph and Dada Zakia
                                           Mwenyekiti Kigoda,Mariam Hilali and Dada Rehema
                                Salum and Mwenyekiti..jamaa anapenda sana kula huyu..lol
    Dada Honoratha na Othman wakiwa makini katika kufuatilia utungwaji wa Katiba ya G.Rutihinda Alumni

SIASA BANA...POLE SANA DR MWAKYEMBE

                                       Dr kazeeka sasa bila kupenda..pole zako mpiganaji
Dr.Mwakyembe akiondoka baada ya kumalizika kwa ibada.Katika salamu zake alisema tangu Octoba 9 mwaka jana alikuwa hajawahi kuweza kuvaa viatu.Kama inavyoonekana katika picha hii,sasa anaweza kuvaa viatu.
 

Tuesday, January 24, 2012

The Woman with Two Vaginas! (Hazel Jones)



Acheni Mungu Aitwe Mungu..Sasa cha ajabu ni hawa jamaa wa XXX wanaotaka kumtumia,Ila yeye anafurahia jinsi alivyo na ameikubali Hali yake

MOJA YA HAZINA ZA GILMAN RUTIHINDA PRIMARY SCHOLL..BIG UP BROTHER KAKOKO



HONGERA DADA YETU ROSE KWA TUZO ULIYO PATA

Haya ni maneno aliyoyaandika Dada yetu Rose katika ukurasa wake wa Facebook..
THANK YOU SANA TENA SANA KWA KUNIWEZESHA MWAKA ULIOPITA MPAKA MWAKA HUU NA KUWEZA KUPATA TUNZO YA ZIFF KAMA MUIGIZAJI WA KIKE BORA TANZANIA NACHUKUA PAGE HII KUWASHUKURU WOTE....LOVE YOU ALL

Sunday, January 22, 2012

Isack Newton

Wakati wangu wa Kusoma maarifa ya jamii pale shuleni kwetu..Huyu alikua nikati ya watu ambao nilikua natamani sana kuwa kama wao kumbe zilikua ni ndoto na utoto ukinisumbua sijui..Salum Siraji

PUNGUZA MATUMIZI YA POSHO SIYO MATUMIZI YA RELI,BARABARA,ELIMU NA AFYA-ZITTO KABWE

Mwezi Disemba mwaka 2011 Waziri wa Fedha na Uchumi alimwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kumwahidi mambo yepi Serikali ya Tanzania itafanya ili kurekebisha Bajeti yake. Utaratibu huu hufanyika kila mwaka kupitia mpango unaoitwa ‘Policy Support Instrument (PSI). Katika barua hiyo Waziri wa Fedha wa Tanzania ameahidi kwamba Serikali itafanya juhudi kupunguza matumizi ili kuweza kupunguza uwiano wa nakisi ya Bajeti na Pato la Taifa (fiscal deficit to GDP ratio) kutoka asilimia 7.2 mpaka asilimia 6.6 ya Pato la Taifa.

Mzee wetu Gilman Rutihinda